Bunge la 11 limeendelea Dodoma, na leo
May 17 2016 ilikuwa ni zamu ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
kuwasilisha hotuba yake pamoja na kuomba kupitishiwa bajeti yake
ijayo. Kazi imefanywa na Waziri wake Makame Mbarawa ambaye ameanza na kuzitoa changamoto za Wizara…
>>‘Katika
utekelezaji wa majukumu yake Wizara inakabiliwa na changamoto
mbalimbali, changamoto hizo ni pamoja na upungufu wa fedha za kutekeleza
miradi ya maendeleo, uzidishaji wa uzito wa magari ya mizigo
unaosababisha uharibifu wa barabara‘
‘Msongamano wa magari katika
jiji la Dar es salaam, uvamizi wa maeneo ya Hifadhi ya Barabara na
Reli, kujenga uwezo wa Makandarasi wazalendo katika kutekeleza miradi ya
maendeleo, ajali za barabarani, wizi wa miundombinu ya uchukuzi
kutokana na biashara ya chuma chakavu n.k’
Mwisho Waziri Mbarawa akaomba fedha…>>>’Katika
mwaka 2016/2017, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inaomba
kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 4,895,279,317,500.00’. Kati ya fedha
hizo, Shilingi 2,212,141,496,500.00 ni kwaajili ya Sekta ya ujenzi‘
‘Shilingi
2,587,333,762,000.00 ni kwa ajili ya Sekta ya Uchukuzi na Shilingi
95,804,059,000.00 ni kwa ajili ya Sekta ya Mawasiliano.






0 comments:
Post a Comment