Tuesday, 24 May 2016

KUPATA TALAKA FUATA HATUA HIZI

Talaka ni haki aliyonayo kila mwanandoa. Kama ilivyo haki ya kufunga ndoa ndivyo ilivyo haki ya talaka pia. Yeyote kati ya wenye ndoa anaweza kuomba talaka.

 Awe mwanamke au mwanaume. Lakini hii ni katika sura ya 29 ya Sheria ya ndoa na si katika imani ya dini yoyote.

 1.TALAKA NININI. 
 Talaka ni amri /tamko maalum la mahakama linalotamka kuhusu kuvunjika kwa ndoa. Hii ndio maana ya talaka lakini kwa mujibu wa sheria. Katika maana hiyo twapata kujua kuwa talaka ni lazima itolewe na mahakama.

Mahakama ndicho chombo chenye dhamana kuu katika kubatilisha ndoa kwa namna ya talaka.

 2. JE UNAWEZA KUOMBA TALAKA MUDA GANI BAADA YA KUFUNGA NDOA.
 Ili uweze kuomba talaka ni lazima ndoa itimize miaka iwili . Huwezi kufunga ndoa mwezi huu halafu mwezi ujao ukakimbilia mahakamani ukitaka talaka. Ndoa ikifikisha miaka miwili basi haki ya talaka inafunguka.

 3. TOFAUTI YA KUTENGANA NA TALAKA. 
 Sio kila kuachana ni talaka. Aina nyingine za kuachana zina sifa za kutengana na sio talaka. Kutengana ni hatua ambapo wanandoa wanaacha kuishi chini ya paa au dari moja. Wanaweza kuishi nyumba moja lakini vyumba tofauti.Halikadhalika wanaweza kuishi nyumba tofauti na hata pakawa mbali ya nchi kwa nchi, mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya,kijiji kwa kijiji n.k.

 Tofauti kubwa kati ya talaka na kutengana ni kuwa katika talaka kunakuwa na tamko maalum kutoka mamlaka maalum linalositisha mahusiano ya ndoa, wakati katika kutengana hakuna tamko lolote kutoka katika mamlaka linalotangaza kuisha au kusitishwa kwa mahusiano ya ndoa. Kutengana kupo kwa aina mbili.

 Kwanza ni kutengana kwa hiari ambapo wanandoa kwa hiari yao wanatengana, na pili ni kutengana kwa kuiomba mahakama kuwatenganisha. Yapo mazingira ambapo kumtenga mwenza kunaweza kuwa kugumu kutokana na mazingira kadha wa kadha na hapo ndipo unapoweza kuiomba mahakama iwatenganishe.

Related Posts:

  • KUPATA TALAKA FUATA HATUA HIZI Talaka ni haki aliyonayo kila mwanandoa. Kama ilivyo haki ya kufunga ndoa ndivyo ilivyo haki ya talaka pia. Yeyote kati ya wenye ndoa anaweza kuomba talaka.  Awe mwanamke au mwanaume. Lakini hii ni katika sur… Read More

0 comments:

Post a Comment