![kichana cha ndizi](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vNZURQouPdD4DazOQr5LGz-3YLWdha6r4ju9QN9os3c41PWUIM8nygjixY9eSHXe4AzoRHatE5kn1aIlARKjESIk3nc1C39rW-3QhoM6KF-Tm3mGMfNM7WKPtRz6FEUjP6ouFiTaI=s0-d)
Ndizi Mbivu zina viburudisho vya
kusaidia kupambana na maradhi kwa mujibu ya wa Utafiti uliofanywa na
Wamarekani na kuwekwa kwenye tofuti ya www.medical.news.
Leo kupitia DODODSO HABARI utaweza kufahamu Faida za Kiafya za kula Ndizi Mbivu:
Husaidia kuponya mfadhaiko wa Akili
(depression), Utafiti unaonesha kuwa tunda hili linauwezo mkubwa wa
kupunguza na kuponya mfadhaiko wa akili kwani watu wenye changamoto hii
hujisikia vizuri baada ya kula ndizi na hii ni kwa sababau ndizi ina
kiburudisho.
Hurekebisha Mzunguko wa Hedhi, ikiwa wewe ni miungoni mwa wanawake wanaopata matatizo ya hedhi unashauriwa kula ndizi mbivu.
Huongeza uwezo wa kufikiri, kwa
wanafunzi hata wasio wanafunzi, ndizi ndio suluhisho la kuongezeza uwezo
wa kufikiri hii ni kwa sababau ndizi ina Potassium ambayo ina uwezo wa
kuamsha fikra.
Kwa wanywaji wa pombe, ndizi mbivu ina
kasumba ya kuondoa ‘hangover’ kwani ni dawa ya haraka ya kuondoa uchovu
unaotokana na unywaji wa pombe.
Huondoa wasiwasi, vidonda vya tumbo, hushusha joto mwilini, hurekebisha mapigo ya moyo na n.k.
TutembeleeKupitia Dododsoblog.com --Facebook Petewilson2016@gmail.com
0 comments:
Post a Comment