Katika kile kinachodaiwa kuwa ni Hapa Kazi Tu, TAASISI ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Katavi
imemfikisha mahakamani Diwani wa Kata ya Katumba, Manispaa ya Mpanda,
Senator Jerith (30) kwa mashitaka ya kushawishi na kupokea rushwa ya Sh
400,000 kutoka kwa mfugaji.
Alifikishwa jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga Tengwa na alikana mashitaka kisha kurejeshwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Jerith, mmoja wa wakimbizi wa Burundi waliopewa uraia wa Tanzania, anadaiwa kupokea rushwa ya Sh 400,000 kati ya Sh milioni moja aliyoiomba kutoka kwa mfugaji Charles Msukuma.
Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Simon Buchwa akisaidiwa na mwenzake, Bhati Haule alieleza kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Mei 11, mwaka huu.
Inadaiwa alimshawishi Msukuma kwamba atamsaidia kutohamisha mifugo yake katika eneo tengefu la makazi ya wakimbizi la Katumba iwapo angekubali kutoa Sh milioni moja.
Mwendesha Mashtaka, Buchwa alidai Jerith alitenda kosa la pili Mei , 12 mwaka huu, katika mgahawa wa Ngandieta ulioko Kata ya Katumba kwa kupokea Sh 400,000, ikiwa ni sehemu ya malipo ya fedha alizokubaliana awali na mfugaji huyo.
Buchwa alidai kuwa mshitakiwa aliomba rushwa ya kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mfugaji huyo asitekeleze amri ya Mahakama ya Mwanzo Katumba iliyoamuru mifugo yote iliyovamia eneo hilo tengefu iondolewe mara moja kwa kuwa iko katika eneo hilo kinyume na sheria.

Share:

0 comments:
Post a Comment