Achana na tetesi za ndoa ya Jay Z na Beyonce kuwa hatarini kuvunjika, sasa wawili hao kumbe wamesharekodi albamu ya pamoja ambayo wamepanga kuiachia hivi karibuni.
April 23 mwaka huu Beyonce aliachia albamu yake ‘Lemonade’ kwa kushtukiza yenye nyimbo kumi lakini kilichowashangaza watu wengi ni baadhi ya mashairi yaliyopo kwenye albamu hiyo yanamtaja Jay Z kuwa aliwahi kumsaliti Queen Bey kwa kutoka na Rachel Roy pamoja na Rita Ora, “Becky with the good hair.”
“This is your final warning / You know I give you life / If you try this s t again / You gon’ lose your wife,” ni baadhi ya mashairi mengine ya Queen Bey yaliyomgusa Jay Z.
Kwa mujibu wa gazeti la New York limeripoti kuwa albamu ya Jay Z na Beyonce imeshakamilika na itaachiwa kwenye mtandao wa Tidal hivi karibuni lakini haijajulikana ni lini wataiachia albamu hiyo huku Beyonce akiwa bado anaendelea na ziara yake ya Formation
0 comments:
Post a Comment